JIHUDUMIE NIDA
Omba Namba ya Malipo (Control Number)
Karibu katika dirisha hili kupata namba ya malipo ya serikali (Control Number)
-
Namba ya malipo (Control Number), hutolewa kwa wateja wanaohitaji kulipia huduma katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Huduma hii kwa sasa hupatikana kwa raia wa Tanzania tu.
Namba ya malipo kwa sasa hutolewa kwa yeyote mwenye uhitaji wa :
Kulipia kitambulisho kilichopotea au kuharibika ili kutengenezewa kingine. Gharama ya huduma hii ni
Tsh 20,000/- kama unabadilisha kwa mara ya kwanza.
Tsh 30,000/- kama unabadilisha kwa mara ya pili.
Tsh 50,000/- kama unabadilisha kwa mara ya tatu au zaidi.
Mhusika anataka kubadilisha taarifa zinazohusisha kubadilisha Kitambulisho cha Taifa.
Kubadilisha taarifa zako NIDA (Kwa maelekezo utakayopewa na maofisa wa NIDA).
Omba namba ya Malipo (Control Number)